Kenya yashinda taji la voliboli Afrika

Image caption Kewnya yashinda taji la mchezo wa Voliboli Afrika

Kenya iliishinda Algeria seti 3-0 katika mechi ya fainali na kuibuka mshindi wa mashindano ya voliboli ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake katika ukumbi wa Kasarani, jijini Nairobi.

Hii ni mara ya tisa na ya tatu mfululizo Kenya kushinda mashindano haya.

Rais wa shirikisho la voliboli Afrika, Amr Elwani, ametangaza Afrika imepewa nafasi nyingine moja hivyo basi timu za Kenya na Algeria zitaiwakilisha Afrika katika mashindano ya kombe la dunia baadaye mwaka huu nchini Japan.

Algeria ilimaliza ya pili ikifuatiwa na Cameroon baada ya kushinda Senegal seti 3-2 mechi ilioamua mshindi wa tatu.

Senegal ilichukua nafasi ya nne ikifuatiwa na Tunisia, Morocco, Mauritius na Botwana ikawa ya mwisho.

Mbali na kuhifadhi ubingwa, wachezaji wanne wa Kenya walituzwa.

Everline Makuto aliteuliwa mchezaji bora, Jane Wacu mpangaji bora, Nafula Wanyama mchezaji huru bora, yaani Libero naye Ruth Jepngetich akawa mzuiaji bora.