Arsenal kumsajili kipa wa Chelsea

Haki miliki ya picha AFP
Image caption KIpa wa Chelsea Petr Cech

Arsenal wanakaribia kuweka makubaliano ya kumsajili kipa wa Chelsea Petr Cech.

Mazungumzo kati ya vilabu hivyo viwili yanaendelea huku kipa huyo akitarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza atakayesajiliwa na Arsenal msimu ujao.

Raia huyo wa Cech aliichezea Chelsea mechi 16 msimu uliopita na amekuwa katika uwanja wa Stanford Bridge kwa takriban miaka 11.

Ameichezea Chelsea mara 300 na kushinda mataji 4 ya ligi,4 ya kombe la FA,mataji 3 ya kombe la ligi ,taji moja la vilabu bingwa Ulaya na taji moja la kombe la Yuropa.