Southgate kuendelea kuwa kocha England

Image caption Kocha Gareth Southgate

kocha wa timu ya vijana ya England chini ya miaka 21 Gareth Southgate amesema anataka kuendelea kuwa kocha wa kikosi hicho.

kauli hiyo ya kocha imekuja baada ya timu yake kuondoshwa katika michuano ya vijana ya ulaya na Itali kwa kuchabagwa mabao 3-1katika mchezo wa mwisho .

"Nina mkataba unaniweka hapa ningependa kubaki ,"alisema Southgate, ambaye mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwaka 2017.

"Nadhani tulikuwa hadithi mkubwa ya mafanikio katika suala la watu binafsi na wamekuja kupitia mpango huo."

Southgate alikwenda katika michuano hiyo ya ulaya bila ya nyota Saido Berahino aliyekua majeruhi , huku akiwakosa Raheem Sterling, Jack Wilshere na Ross Barkley ambao wangeweza kukisaidi kikosi hicho lakini kutokana kuwa wachezaji wanaokichezea kikosi cha kwanza cha wakubwa waliachwa.