Japan yaichapa Uholanzi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Timu ya wanawake ya mpira wa miguu

Timu ya taifa ya Japan imekua timu ya mwisho kufuzu kwa robo fainali katika michuano ya kombe la dunia la wanawake.

Japani imeibuka kidedea kwa ushindi. Mabao 2-1

Mabao ya japani yaliwekwa kimiani Saori Ariyoshi dakika ya 10 huku kiungo Mihuzo Sakaguchi Akipachika bao la pili

Huku bao pekee la kufutia machozi la waholanzi likiwekwa kambani na mshambuliaji Van de ven.

Kwa ushindi huo Japan itawakabili Australia katika mchezo wa robo fainali ya tatu itayokaopigwa Tarehe 27.