Anelka kuifunza kilabu ya Mumbai

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nicholas Anelka katikati

Aliyekuwa mchezaji wa vilabu vya Arsenal na Chelsea Nicolas Anelka amechaguliwa kama mkufunzi wa klabu ya Mumbai City.

Anelka mwenye umri wa miaka 36 aliichezea klabu hiyo ya ligi kuu nchini India chini ya ukufunzi wa aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Manchester City Peter Reid.

''Alituvutia sisi sote na ufundi wake pamoja na ujuzi wa hali ya juu alionao'',alisema mmiliki wa kilabu hiyo ambaye pia ni mwigizaji nyota wa Bollywood Ranbir Kapoor.

Anelka alikuwa mchezaji mkufunzi katika kilabu ya Shanhai Shenhua mwaka 2012.

Raia huyo wa Ufaransa alifanikiwa kufunga mabao mawili pekee katika mechi saba alizocheza katika msimu wake wa kwanza mjini Mumbai lakini anarudi katika kilabu hiyo kama mchezaji ambaye anafaa kulipwa mshahara mkubwa.