Barcelona kumsajili Pogba

Haki miliki ya picha
Image caption Paul Pogba

Mgombea wa wadhfa wa urais katika klabu ya Barcelona Joan Laporta anasema kuwa mabingwa hao wa Ulaya watajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Juventus Paul Pogba iwapo atachaguliwa.

Ripoti zinasema kuwa kilabu ya Barcelona ilijaribu kumsajili raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 ambaye aliisaidia Juventus kushinda ligi ya Serie A na kufika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.

''Kuna mchezaji tunayempenda sana -Paul Pogba. Tunamjua ajenti wa mchezaji huyo na hilo na swala muhimu katika oparesheni zetu. Tutajadiliana na wakala wake pamoja na klabu ya Juventus'',. Alisema Laporta.

Siku ya Jumatano ,vyombo vya habari nchini Uhispania na Italy vilisema kuwa Barcelona imetoa kitita cha yuro milioni 80 kwa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United ambaye pia anahusishwa na uhamisho katika vilabu vya Chelsea na Manchester City.