Podolski kusajiliwa na Galatasaray

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Lucas Podolski

Mshambuliaji Lukas Podolski ameondoka Arsenal na anatarajiwa kujiunga na Galatasaray kulingana na kilabu hiyo ya Uturuki.

Kilabu hiyo inasema kuwa mchezaji huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 30 atakamilisha uhamisho wake siku ya jumamosi baada ya kufanyiwa ukaguzi wa matibabu.

Podolski alijiunga na timu ya Arsenal kutoka kilabu ya Ujerumani ya FC Koln mwaka 2012 kwa kitita cha pauni milioni 11 na kuweza kuifungia Arsenal mabao 31 kati ya mechi 82 alizochezea the Gunners.

Aliisaidia Arsenal kushinda kombe la FA mwaka 2013 lakini akaichezea kilabu ya Inter Milan msimu uliopita kwa mkopo.

Uwezo wake wa kupata nafasi ya kuiwakilisha Gunners ulipungua baada ya meneja Arsene Wenger kuwasajili wachezaji Mesut Ozil,Alexis Sanchez na Danny Welbeck.