Fainali:Japan kuchuana na Marekani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wachezaji wa Japan baada ya kuishinda Uingereza katika nusu fainali

Mabingwa watetezi Japan watajaribu kulihifadhi taji lao la kombe la dunia upande wa wanawake wakati ambapo wanakutana na Marekani kwa kipute cha fainali ya kombe hilo kwa mra ya pili mfululizo.

Japan iliishinda Uingereza 2-1 katika nusu fainali na kupelekea marudio ya fainali ya mwaka 2011 walipoichapa Marekani 3-1 kupiti mikwaju ya penalti baada ya mechi kukamilika 2-2.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Japan wakikabiliana na Uingereza

Lakini katika mashindano ya Olimpiki mjini London,Marekani ilichukua dhahabu ilipoishinda Japan 2-1 katika fainali.

''Ni mechi ya kulipiza kisasi kwa timu zote mbili'',alisema beki Saki Kumagai.''Ukilinganisha na miaka minne iliopita ama hata miwili iliopita wachezaji wote wa timu yetu wamekuwa.Itakuwa mechi ambapo sisi sote tutaonyesha tulivyoimarika''.