Nigeria yampiga kalamu mkufunzi Keshi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Stephen Keshi na kipa Enyeama

Stephen Keshi amepigwa kalamu kama kocha wa timu ya Nigeria The Super Eagles na nafasi yake kuchukuliwa na Shaibu Amodu kulingana na shirikisho la soka nchini Nigeria NFF.

Hatua hiyo inajiri wiki mbili tu baada ya shirikisho hilo kuanzisha uchunguzi kuhusu ripoti kwamba Keshi alituma ombi la kutaka kuifunza Ivory Coast licha ya kuwa na kandarasi halali na Nigeria.

Keshi hivi majuzi alidai kwamba wakala ambaye hakumtaja aliwasilisha jina lake bila ruhusa yake kuwania wadhfa huo wa timu ya Ivory Coast.