Kocha wa Simba ajinasibu kutawala soka.

Image caption kocha wa Simba Dylan Kerr akiwa kazini.

Kocha mpya wa Simba, Muingereza Dylan Kerr amesema ana imani timu ya Simba itakuwa tishio msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.

Simba ilimaliza nafasi ya tatu ligi kuu, Yanga ikiwa bingwa na Azam ikishinda nafasi ya pili.

Kocha huyo Muingereza tayari ameanza kazi ya kuifundisha timu hiyo ambayo imeanza mazoezi kwa ligi kuu inayotegemewa kuanza mwezi Agosti.Kocha huyo amesema ana Imani Simba itakuwa klabu bora barani Afrika na anaomba muda ili aifikishe mbali.

“Naomba wapenzi wa Simba wawe na Subira ili timu ifanye mafanikio”.“Nahitaji ushirikiano katika kila kutoka kwa viongozi na wapenzi ili tufanikiwe”, amesema kocha huyo, anayerithi mikoba ya Mserbia Goran Kopunovic, ambaye alikataa kuendelea na Simba baada ya kudai dau nono.