Serena na Venus kuchuana-Wimbledon.

Image caption Serena Williams akiwa uwanjani hana masihara.

Serena Williams na nduguye Venus wanatarajiwa kuvaana leo katika mchezo wa mzunguko wa nne wa mashindano ya Wimbledon.

Wanadada hao raia wa Marekani leo itakuwa ni mara yao ya 26 kukutana huku Venus ambaye ndio mkubwa akijaribu kurejea katika kiwango chake baada ya kudhoofika kwa maradhi .

Kutokana na udugu wao, Serena amesema uhusiano wao ni muhimu zaidi kuliko kipute hicho, japo anauhakika kuwa mchezo huo utakuwa mzuri na chochote kitakachojiri kitabaki hapo hapo uwanjani.Naye Andy Murry atamenyana na Ivo Karlovic katika mashindano hayo hayo.