Kiiza atua rasmi Simba

Image caption Kiiza mwenye jezi za kijani

Timu ya Simba imesema Mganda Hamisi Kiiza atakuwa chachu ya mafanikio katika msimu ujao baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili Kiiza amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba ya Tanzania katika msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.

Kiiza aliichezea timu ya Yanga, ambayo ni mahasimu wa Simba katika msimu uliopita na baadae klabu hiyo kuamua kuachana naye. Habari kutoka SImba zinasema wana imani mchezaji huyo ataisaidia timu hiyo iliyomaliza nafasi ya tatu katika msimu uliopita na ikiwa na kiu ya kushiriki michuano ya kimataifa, baada ya kutoshiriki kwa miaka kadhaa. Awali, Kiiza alihusishwa na timu ya Mbeya City lakini msemaji wa Simba, Haji Manara amenukuliwa akisema wamemalizana na Mganda huyo, aliyejiunga kama mchezaji huru