Voliboli:Kenya yafuzu kwa nusu fainali

Image caption Voliboli:Kenya yafuzu kwa nusu fainali

Kenya imefuzu kwa mkumbo wa nusu fainali ya mchuano wa voliboli ya wanawake ya Grand Prix baada ya kuwanyamazisha Algeria seti 3-2 kwao

Kenya ilimaliza katika nafasi ya tatu baada ya kushinda Algeria seti 3-2 na hivyo basi kumaliza mechi zake za raundi ya pili bila kushindwa katika mashindano ya Grand Prix ya mpira wa voliboli kwa upande wa wanawake.

Columbia waliibuka videdea katika kinyang'anyiro hicho huko Algeria walipojizolea jumla ya pointi 15.

Kenya ilimalaiza na pointi 10, sawa na Cuba iliyomaliza ya nne lakini kwa Kenya ilishinda mechi nne na Cuba mechi tatu.

Kenya sasa itapambana na Australia mechi ya nusu-fainali jumamosi hii huku Peru ikimenyana na Columbia katika ile nusu fainali nyingine.

Wadadisi wanaipigia upatu Kenya kwani tayari walikuwa wamewabana Australia katika mechi za mchujo.

Australia imemamaliza ya mwisho kundi la tatu.

Lakini imefuzu kwa nusu-fainali kama mwenyeji.

Mechi kati ya Kenya na Algeria ilikua ya kukata na shoka kwani wenyeji walishinda seti ya kwanza alama 25-20.

Kenya ilishinda seti ya pili seti alama 25-15, huku Algeria ikinyakua seti ya tatu alama 25-23.

Image caption Australia imemamaliza ya mwisho kundi la tatu.

Wasichana hao wa Kocha David Lung'aho walijifurukuta na kuwazima wapinzani wao alama 25-13 katika seti ya nne kabla ya kutamatisha kivuno hicho cha pointi kwa kushinda alama 15-13.

Mercy Moim na Everline Makuto ni miongoni mwa wachezaji wa Kenya waliotia fora kwenye mechi hiyo na kuiwezesha Kenya kushinda Algeria nyumbani kwa mara ya kwanza.

Kenya ilijihakikishia hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kuishinda Mexico na Australia seti 3-0 katika mechi za hapo awali.

Bado haijantangazwa nani mpinzani wao katika mechi ya nusu-fainali.

Columbia ilishangaza wengi kwa kushinda mabingwa wa zamani wa dunia Cuba seti 3-1 na kuchukua nafasi ya kwanza ikiwa na jumla ya pointi 15 ikifuatiwa na Peru iliyojizolea alama sawa na hizo.

Licha ya kupoteza mechi hiyo mchezaji chipukizi wa Cuba Melissa Vargas alimaliza mechi hiyo akiwa mfungaji bora zaidi na pointi 31.