Oliseh kuwa kocha wa Nigeria ?

Image caption Oliseh anafanya mazungumzo na shirikisho la soka la Nigeria NFF kwa nia ya kutangazwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Nigeria.

Je, Sunday Oliseh ndiye atakaye kuwa kocha mpya wa Nigeria ?

BBC imebaini kuwa kiungo huyo wa kati wa zamani wa Super Eagles ya Nigeria, Sunday Oliseh anafanya mazungumzo na shirikisho la soka la Nigeria NFF kwa nia ya kutangazwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Nigeria.

Nahodha huyo wa zamani wa Super Eagles mwenye umri wa miaka 40 aliingoza timu hiyo katika mechi 63 za kimataifa.

Kwa mujibu wa mwandani wetu anatarajiwa kutangazwa karibuni kuwa kocha mpya.

Image caption Oliseh alikuwa miongoni mwa kikosi cha taifa kilichotwaa kombe la mataifa ya Afrika mwaka wa 1994 na kisha nishani ya dhahabu ya olimpiki mwaka wa 1996 .

NFF ililazimika kufanya bidii ilikuziba pengo lililoachwa wazi na Stephen Keshialiyefutwa kazi mwishoni mwa juma.

Oliseh alikuwa miongoni mwa kikosi cha taifa kilichotwaa kombe la mataifa ya Afrika mwaka wa 1994 na kisha nishani ya dhahabu ya olimpiki mwaka wa 1996 .

Oliseh vilevile alikuwa katika kikosi kilichoiwakilisha Nigeria katika kombe la dunia la mwaka wa 1994 na 1998.

Super eagles ilifuzu katika mkumbo wa 16 bora katika mashindano hayo mawili.

Oliseh anakumbukwa kwa bao lililoisaidia Nigeria kuibana Uhispania katika mechi za makundi.

Image caption Oliseh atachukua hatamu kutoka kwa mkurugenzi wa kiufundi wa NFF Shaibu Amodu na kocha msaidizi Salisu Yusuf.

Kizazi chake kinatajwa na wengi kuwa maarufu zaidi katika historia ya soka ya nchi hiyo kwa pamoja na Jay-Jay Okocha, Nwankwo Kanu na Finidi George.

Oliseh amekuwa akihudumu kama mtangazaji wa kandanda mbali na kuwa mshauri wa FIFA wa maswala ya kiufundi.

Japokuwa Oliseh hana tajriba ya kufunza timu ya taifa aliwahi kuifunza timu ya daraja la pili la Ubeljiji Vervietois kati ya mwaka wa 2008 na 2009.

Iwapo atatangazwa kuwa kocha wa Nigeria Oliseh atachukua hatamu kutoka kwa mkurugenzi wa kiufundi wa NFF Shaibu Amodu na kocha msaidizi Salisu Yusuf.