Murray atinga nusu fainali Wimbledon

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Andy Murray akipunga mkono wa shukrani

Muingereza Andy Murray ameingia nusu fainali yake ya sita kwenye michuano ya Wimbledon katika kipindi cha miaka saba baada ya kumbwaga Vasek Pospisil kwa ushindi wa set 6-4 7-5 6-4 kwenye mchezo uliodumu kwa saa mbili na dakika 13.

Kwa matokeo hayo sasa Murray atavaana na Roger Federer kwenye mchezo utakaopigwa kesho. Federer ametinga katika hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kumshinda Gilles Simon raia wa Ufaransa kwa jumla ya set 6-3 7-5 6-2.

Naye bingwa nambari moja ulimwenguni katika mchezo wa tennis Novak Djokovic atamenyana na Richard Gasquet baada ya kumshinda Marin Cilic kwa set 6-4 6-4 6-4.