TFF: Messi ni mchezaji huru

Image caption Ramadhani Singano wa Simba,wa pili kulia akishangilia.

Utata uliogubika mkataba wa mchezaji Ramadhani Singano maarufu “Messi” dhidi ya timu yake ya Simba inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara umefikia tamati baada ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania kusema mchezji huyo ni huru .Uamuzi huo unakuja baada ya Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji iliyochini ya TFF kuvunja mkataba kati ya Messi na Simba.

Mmoja wa viongozi wa kamati hiyo amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa mkataba huo umevunjwa kwa kuwa Simba ilishindwa kutekeleza vipengele kadhaa vya mkataba.

Messi, moja ya wachezaji wazuri wanaochipukia, aliingia katika mgogororo wa kimkataba na maslahi na klabu yake ya Simba, ambayo lilidai yeye ni mchezaji wao halali mpaka msimu ujao, wakati mchezaji mwenyewe akisema mkataba wake umeisha msimu huu. Simba inadaiwa kukiuka baadhi ya vipendegele katika mkataba huo, likiwemo suala la bima na kodi ya pango ya nyumba