Azam yawapigisha kwata Ruvu JKT

Image caption Azam wakifurahia ushindi

Goli lililofungwa na Muivory Coast, Kipre Tchetche lilitosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ta timu ngumu ya JKT Ruvu katika mchezo wa kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kombe la Kagame baadae mwezi huu.

Ikijaribu mfumo mpya wa 3-5-2, Kipre alifunga goli gilo la pekee dakika moja kabla ya kumalizika kwa mchezo huo akitokea benchi kuchukua nafasi ya Mrundi Dedier Kavumbagu .

Mechi hii ya kusisimua ilichezwa kwenye uwanja wa Chamazi complex, JKT Ruvu ilijitutumua na kucheza soka safi lakini habati ya kupata goli haikuwa upande wao. Kipre alifunga goli hilo la Azam FC dakika nne tuubaada ya kuingia akiunganisha krosi ya kiungo aliyecheza vizuri sana Salum Abubakar.

Ingawa mechi hiyo ilikuwa na lengo la kumjaribu golikipa mpya toka Ivory Coast, Vincent Atchouailou de Paul Angban aliyewahi kudakia timu ya vijana ya klabu bingwa England, Chelsea FC lakini benchi la ufundi lililazimika kumuacha kumpa muda wa kujiandaa kutokana na kutoka likizo na kuhitaji mazoezi ya kusaka wepesi kabla hajapewa muda wa majaribio.