Fifa yataja viwango vya ubora wa soka

Haki miliki ya picha Reuters

Tanzania na Uganda zimeshuka katika viwango ya FIFA vilivyotolewa Alhamisi huku Kenya , Sudan na Rwanda zikipanda.

Uganda, ambayo ilikuwa nafasi ya 71, imeshuka nafasi mbili na sasa ni ya 73 wakati Tanzania, imeshuka nafasi 12 na sasa ni ya 139.

Licha ya kushuka, Uganda, ambayo hivi karibuni imeitoa Tanzania katika kugombania nafasi ya kucheza fainali za CHAN mwakani nchini Rwanda, ndio nchi iliyo juu katika viwango vya FIFA kwa nchi za Afrika ya Mashariki.

Kushuka kwa Tanzania kunatokana na kufungwa na Uganda 4-1 katika michuano ya CHAN na kufungwa na Misri 3-0 katika mechi ya kwanza ya kugombania kufuzu kucheza fainali za AFCON.

Kenya imepanda nafasi saba na sasa ni ya 116 katika viwango hivyo ya Dunia. Rwanda ipo nafasi ya 78, ikipanda nafasi 16 wakati Sudan ikiwa nafasi ya 90, ikipanda nafasi 18. Burkina Faso (72), , Botswana (120) na Comoros (187).

Algeria ndio timu inayoongoza katika viwango vya FIFA kwa Afrika ikiwa nafasi ya 19. Timu ya Agentina, lich ya kufungwa na Chile katika fainali za Copa America, imepanda na kuwa timu ya kwanza katika viwango va FIFA, ikiitoa Ujerumani. Tano bora za viwango vya FIFA ni Argentina, Germany, Belgium, Colombia na Uholanzi.