Mo Farah avunja ukimya

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Mo Farah

Mwanariadha Mo Farah amewajibu wakosoaji wake kwa vitendo baada ya kushinda katika mbio za mita elfu tano za Diamond huko mjini Lausanne nchini Switzerland.

Farah ameibuka kidedea katika mbio hizo huku akitumia muda wa dakika 13 na sekunde 11.77 na kusema kuwa hayo ni majibu juu ya tuhuma zinazomkabili kocha wake Alberto Salazar kuhusiana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

Mo Farah hakutuhumiwa kufanya makosa na alikwisha karibisha wachunguzi kutoka Uingereza na mawakala wa kupinga matumizi ya dawa hizo kutoka Marekani ili wakamfanyie uchunguzi huku kocha wake Salazar akipinga kuhusika na utumizi wa dawa hizo.

Sasa mwanariadha huyo anategemea kushiriki katika mbio za mita elfu moja mia tano huko mjini Monaco mnamo July 17.