Gerrard:Sterling huenda akaondoka Anfield

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gerrard

Aliyekuwa nahodha wa kilabu ya Liverpool Steven Gerrard amekasirishwa na mchezaji Raheem Sterling huku akimsifu Jordan Henderson kwa kuwa nahodha mpya wa kilabu hiyo.

Sterling amekosa mazoezi kupiti ugonjwa na hataki kusafiri na kilabu hiyo kwa ziara ya likizo baada ya pauni milini 40 kutoka klabu ya Manchester City kukataliwa.

''Jordan amekuwa mwaminifu kwa kilabu hiyo kwa kuweka kandarasi mpya na namtakia mazuri'',alisema Gerrard mwenye umri wa miaka 35.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Sterling

Akizungumza na BBC mchezaji huyo ambaye ameihama kilabu hiyo alisema kuwa hadhani kwamba Sterling atasalia katika uwamnja wa Anfield.

Baada ya kuiambia Liverpool kwamba hataki kusafiri na kikosi cha Liverpool kwa ziara ya mashariki ,mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alikosa kufanya mazoezi siku ya jumatano na alhamisi baada ya kupiga simu na kusema anaugua.