Alexis Sanchez anahitaji kupumnzika

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Alexis Sanchez kukosa mechi kikosi cha Arsenal

Alexis Sanchez anaweza kukosa mechi ya kwanza ya msimu katika kikosi cha Arsenal.

Kocha Arsene Wenger anasema Mshambuliaji huyo anaweza kuukosa mchezo huo mara baada ya kuwa ameisaidia timu yake ya Chile kutwaa taji la Copa America kwa kuwa atajiunga nao tarehe 3 mwezi ujao na inaweza kuchukua wiki tatu mchezaji kuwa fit tena. Sanchez ataukosa mchezo wa ngao ya jamii wa tarehe mbili dhidi ya Chelsea.