Di Maria kujiunga na PSG

Haki miliki ya picha AP
Image caption Di Maria

Mchezaji wa Manchester United Angel Di Maria amewaeleza wakuu wa kilabu ya PSG nchini Ufaransa kwamba anataka kujiunga na kilabu hiyo.

Kulingana na gazeti la Le Perisien mazungumzo kati ya vilabu hivyo viwili yanaendelea huku wakidaiwa kukubaliana kwa kitita cha pauni milioni 42.8.

Di Maria amekosa kuichezea Man United katika ziara ya timu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu ujao nchini Marekani akidaiwa kupumzika baada ya kushiriki katika kombe la Copa America.