Sunday Oliseh ndiye kocha mpya wa Nigeria

Image caption Sunday Oliseh

Nigeria imemchagua aliyekuwa mchezaji wa Nigeria Sunday Oliseh kocha mpya wa Nigeria.

Oliseh mwenye umri wa miaka 40 ameweka kandarasi ya miaka mitatu na anamrithi Stephen Keshi ambaye alifutwa kazi mwanzo wa mwezi Julai.

''Tuna vipawa vya kubadilisha hatma yetu ili kurudisha heshima tuliokuwa nayo na kuhakikisha kuwa tunapata matokeo mazuri'',alisema Oliseh.

''Hii ni kazi kubwa barani Afrika,tukiungwa mkono na kila mtu tunaweza kuisadia Super Eagles kupaa tena''.

Oliseh aliyeichezea Nigeria mara 63 na kuisadia kushinda kombe la Afrika mwaka 1994 pamoja na dhahabu katika mashindano ya Olimpiki mwaka 1996 anachukua wadhfa huo wakati ambapo Nigeria wanapambana kuimarika nje na hata ndani ya uwanja.