Real Madrid:Sergio Ramos haondoki

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Sergio Ramos

Mchezaji Sergio Ramos anayelengwa na Manchester United msimu huu hataondoka Real Madrid kulingana na mkufunzi Rafael Benitez.

Ombi la United la kutaka kumsajili beki huyo kwa kitita cha pauni milioni 28 lilikataliwa na Real Madrid ambayo inamwinda kipa wa Manchester United David De Gea.

Lakini Benitez alisema:''Ninamuona Sergio kama kiungo muhimu cha timu yetu. Ni mshindi na hicho ndicho tunachokitaka''.

Rais wa Real Madrid tayari amesema kuwa Ramos atasalia katika kilabu hiyo.

Mkufunzi huyo wa zamani aliyeifunza Liverpool na Chelsea ambaye alisajiliwa na Real Madrid mwezi Juni,aliongezea:''Nimeongea na Ramos kwa urefu msimu huu kuhusu hatma yake''.