FIFA:Rais wa soka Bolivia akamatwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Soka nchini Bolivia Carlos Chavez

Rais wa shirikisho la soka nchini bolivia Carlos Chavez amekamatwa kama sehemu ya uchunguzi unaohusu ufisadi.

Uchunguzi huo ulichochewa na hatua za idara ya mahakama nchini Marekani kuhusu ufisadi ambao umekuwa ukiendelea ndani ya shirikisho la kandanda duniani FIFA.

Bwana Chavez ndiye mueka hazina wa shirikisho la kandanda la nchi za Amerika ya Kusini CONMEBOL

Alikamatwa katika mji wa Sucre nchini Bolivia baada ya kutoa ushahidi kwenye uchunguzi unaohusu ufisadi katika shirikisho la kandanda nchini Bolivia.

Mameneja kadha wa kandanda nchini humo nao wanafanyiwa uchunguzi.