FIFA:Webb akanusha mashtaka ya ufisadi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Baadhi ya washukiwa ufisadi katika shirikisho la soka la FIFA

Makamu wa rais wa zamani wa shirikisho la Soka duniani FIFA Jeffery Webb amekanusha mashtaka ya ufisadi mbele ya mahakama mjini New York.

Ameachiliwa kwa dhamana ya dola milioni kumi, kwa sharti kuwa asisafiri umbali wa kilomita thelathini kutoka mahakama hiyo na mienendo yake yote inachunguzwa kwa njia ya elektroniki.

Bwana Webb alirejeshwa kwa lazima nchini Marekani wiki iliyopita kujibu mashtaka, ambapo anashutumiwa kupokea mamilioni ya dola kama rushwa ili kutoa haki za mauzo na matangazo ya biashara wakati wa mchezo huo.

Yeye ni miongoni mwa maafisa wengine sita wa shirikisho hilo waliokamatwa mjini Zurich mwezi Mei kufuatia uchunguzi wa FBI wa ufisadi ndani ya shirikisho hilo.

Washukiwa hao wengine bado wanapinga kurejeshwa Marekani kwa kesi hiyo.