Cambiasso akataa kurejea Leicester City

Haki miliki ya picha PA
Image caption Esteban Cambiasso

Kiungo wa Argentina Esteba Cambiasso amekataa mkataba wa kubaki timu ya Leicester City ya England.

Kiungo huyo mwenye miaka 34 alijiunga na Foxes kwa mkataba mwaka mmoja uliomalizika mwezi uliopita.

Kocha mpya Claudio Ranieri amesema alizungumza na Cambisso kuhusu mkataba mpya na alijaribu kushawishi " Rudi nyumbani".

Hata hivyo mchezaji huyo wa zamani wa Inter Milan na Real Madrid alisema katika taarifa yake kwamba " Nimeamua kutosaini mpya mkataba na Leicester City.