Wenger:Walcot kusalia Arsenal

Haki miliki ya picha epa
Image caption Walcot

Mshambuliaji wa Arsenal, Theo Walcott anakaribia kuongeza mkataba wake na klabu hiyo hadi mwaka wa 2019.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amefichua kuwa Walcott atasaini kandarasi mpya na timu hiyo huku akiwa amesalia na mwaka mmoja tu katika klabu hiyo.

Walcott mwenye umri wa miaka 26 aliifungia Arsenal goli la kipekee dhidi ya Wolfsburg na kuiwezesha Arsenal kuondoka na kombe la Emirates.

Aidha, kipa wa Poland, Scszesny yuko mjini Roma, nchini Italia kujiunga na As Roma baada ya kupoteza nafasi yake kwa aliyekuwa kipa wa Chelsea, Petr Cech.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Mkufunzi Arsene Wenger

Scszesny anasubiri ukaguzi wa kimatibabu kabla ya kujiunga na timu hiyo kwa njia ya mkopo.

Meneja wa Arsenal, Wenger, amekuwa chini ya shinikizo kali kuimarisha timu hiyo ili kuleta ushindani mkali kwenye ligi ya Uingereza pamoja na ligi ya vilabu bingwa Ulaya msimu huu.

Arsenal inalenga kuondoka na taji la tatu kabla ya msimu kuanza itakapochuana na Chelsea uwanjani Wembley wikendi ijayo.