Van Gaal:'Nitaondoka Man U kukaa na mke'

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Van Gaal

Meneja wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa huenda akaondoka katika kilabu ya Manchester United mwisho wa kandarasi yake ya miaka mitatu ili kutimiza ahadi aliotoa kwa mkewe.

Alipoulizwa iwapo ataongeza kandarasi yake katika uwanja wa Old Traford ,raia huyo wa Uholanzi ameiambia BBC kwamba ataondoka mwisho wa kandarasi yake mwaka 2017.

''Nilimuahidi mkewe wangu.hatuna miaka mingi iliosalia,na hiyo ndio sababu'', alisema menejea huyo mwenye umri wa miaka 63.

''Nimefanya kila kitu katika maisha yangu kama mkufunzi''.Alipulizwa iwapo kuna uwezekano wa yeye kusalia katika kilabu hiyo,alijibu kwamba haweza kutoa jibu lolote kwa kuwa mkewe amekasirika sana.

''Nakiri kwamba nilimwambia kuwa nitaastaafu ifikiapo miaka 55 lakini nikiwa na miaka 63 bado naendelea na ukufunzi na wiki ijayo nitakuwa na miaka 64''alisema meneja huyo.