Platini kuwania uongozi wa FIFA

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Platini

Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini anatarajiwa kutangaza azma yake ya kuwania urais wa FIFA baadaye wiki hii.

BBC imebaini kwamba Platini baada ya kuungwa mkono na mashirikisho ya soka kutoka mabara manne atakuwa mgombea wakati uchaguzi wa shirikisho la soka duniani utakapofanyika februari 26 mwaka ujao.

Platini mwenye umri wa miaka 60 huenda akatangaza azma yake siku ya jumatano.

Raia wa Uswizi Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79 amekuwa akilisimamia shirikisho hilo tangu mwaka 1998.

Anastaafu mwezi Februari kutokana na kashfa ya ufisadi katika shirikiso la FIFA.

Na Platini anapigiwa upatu kumrithi.

Anaungwa mkono na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA,shirikisho la soka kusini mwa Marekani Conmebol,shirikisho la kaskazini,America ya kati na visiwa vya Carebean, Concacaf na lile la Asia AFC.