Irvine: Berahino haendi Tottenham

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kocha wa zamani wa Westbrom,Alan Irvine

Kocha wa zamani wa Westbrom Alan Irvine amesema Saido Berahino hayupo tiyari kujiunga na miamba ya kaskazini mwa London Tottenham Hotspur.

Chipukizi huyo wa timu ya Taifa ya Uingereza chini ya miaka 21 ambaye msimu uliopita alipachika mabao 14 amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Tottenham kwa muda mrefu.

''Yupo tayari kucheza katika timu kubwa iliyo kwenye nne bora?,nafikiri bado ''Irvine aliiambia BBC.

''Nimekuwa nikisema kuwa kama Saido atajikita zaidi katika kusakata kabumbu ataendelea sana''

Irvine aliyeingoza Baggies katika nusu ya msimu uliopita alimtumia Berahino katika michezo 22 huku chipukizi huyo akifumania nyavu mara 8.

''Ni muhimu sana acheze. Yupo katika kiwango kizuri ambacho anahitaji kucheza kila mara. Ana kipaji na maendeleo yake ni mazuri''. Aliongeza mwalimu wa sasa wa Westbrom Tony Pulis