Bottas asema sihami ng'oo Williams

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Valtteri Bottas dereva wa magari ya langa langa

Dereva wa magari ya langa langa Valtteri Bottas amesema amechoshwa na uvumi kwamba anampango wa kuhamia kampuni ya Ferrari.

Bottas amesisitiza kwamba jambo kubwa analolilenga kwa sasa si kuhama bali ni kushinda michuano ijayo ya magari ya Grand Prix.

Bottas mwenye umri wa miaka 25 anatajwa kwamba atamrithi Kimi Raikkonen katika timu ya Italia katika michuano ya mbio za magari ya mwaka 2016.

Hata hivyo Bottas ambaye ameitumikia timu yake ya Williams kwa mhula wa tatu sasa,anasema jambo moja la msingi analowaza kwa sasa ni kuisaidia timu yake ya sasa na kuhakikisha inashinda.

“Unapokuwa ndani ya gari unaendesha hakuna uvumi wowote unaoweza kuwaza ,zaidi ya kufikiria jambo moja tu la ushindi.

Kampuni ya Mercedes kwa muda imekuwa kinara katika mashindano hayo yam bio za magari,langalanga kwa msimu wa kwanza katika ndani ya mwaka huu.