CECAFA:Gor Mahia kuchuana na Azam

Image caption wachezaji wa Azam

Kilabu ya Azam kutoka Tanzania imefuzu katika fainali ya ombe la Kagame CeCAFA baada ya kuindoa KCCA ya Uganda kwa bao moja kwa bila katika mechi ya nusu fainali ya pili iliochezwa katika uwanja wa kitaifa wa Dar-es-Salaam nchini Tanzania.

Hatua hiyo inaaminisha kwamba Kilabu ya Gor Mahia ya Kenya itakabiliana na Azam katika fainali ya Kombe la CECAFA.

Azam ilihitaji bao la dakika za mwisho lililofungwa na Farid Musa kuilaza KCCA kutoka Uganda na kufuzu katika awamu ya kilele cha kombe hilo.

Image caption Mshambuliajai wa Gor Mahia Michael Olunga

Fainali hiyo itachezwwa siku ya jumapili katika uwanja huohuo.

Gor Mahia ilifuzu katika fainali baada ya kuicharaza kilabu ya Al Khartoum kutoka Sudan 3-1 kupitia mabao yaliofungwa na Michael Olunga,Innocent Wafula na Meddie Kagere.

K'Ogalo sasa itashiriki katika fainali ya kwanza tangu mwaka 1985.