Nadal atwaa ubingwa wa Hamburg

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nyota wa mchezo wa Tenisi, Rafael Nadal

Nyota namba kumi kwa ubora wa mchezo wa tenesi duniani Rafael Nadal ametwaa ubingwa wa michuano ya wazi ya hamburg.

Nadal alimshinda mpinzani wake Fabio Forgnini raia wa Italia kwa seti 7-5 7-5 na kutwaa taji lake la tatu kwa mwaka huu.

Hii ilikua ni michunao ya kwanza mikubwa kushiriki kwa nyota huyu tangu aliposhiriki michuano ya wazi ya Wimbledon.

Na kwa upande wa wachezji wawili wawili Mwingereza Jamie Murray na John Peers wa Australia wameibuka mabingwa wa michuano hiyo ya wazi baada ya kuwagaragaza wapinzao wao Juan Cabal Na Robart Farah

Nyota hawa walianza kwa kupoteza seti ya kwanza kwa 2-6 kisha wakashinda kwa seti 6-3 na 10-8, Jamie murray na John Peers walicheza kama pacha katika michuano ya wazi Wimbledon