Edin Dzeko kujiunga na Roma

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Dzeko

Mshambuliaji wa kilabu ya Manchester City Edin Dzeko anatarajiwa kujiunga na kilabu ya ligi ya Serie A, Roma baada ya kilabu hiyo kukubali uhamisho wa kitita cha pauni milioni 14.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutoka Bosnia Hacegovina alijiunga na City kutoka Wolfsburg mnamo mwezi Januari mwaka 2011 kwa kitita cha pauni milioni 27.

Alitia sahihi kandarasi mpya katika uwanja wa Etihad msimu uliopita.

Hatahivyo Meneja Manuel Pelegrini alikiri hivi majuzi kwamba Dzeko alitarajiwa kuondoka kufuatia ununuzi wa Raheem Sterling kutoka kilabu ya Liverpool.