Audi:Real Madrid yaichapa Tottenham

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gareth Bale aliifunga bao la pili timu yake ya zamani, Tottenham

Miamba ya soka wa Hispania Real Madrid wameichapa timu ya Tottenham kwa mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali wa kikombe cha Audi.

Mchezo uliofanyika katika uwanja wa Allianz Arena ikiwa ni mchezo wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi barani ulaya.

Mabao ya Real Madrid yaliwekwa kiamiani na James Rodriguez, huku mshambuliaji wa zamani wa timu ya Tottenham Gareth Bale akifunga bao la pili.

Katika mchezo wa pili wa michuano hii,Bayern Munich iliichapa Ac Millan kwa mabao 3-0

Hivyo fainali itazikutanisha Real Madrid na Bayern Munich mchezo utaokochezwa jumatano

Michuano hii ya Audi ilizishirikisha timu nne wenyeji Bayern Munich, Real Madrid,AC Milan na Tottenham.