Di Maria ajiunga na PSG ya Ufaransa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Di Maria

Klabu ya Paris St-Germain imekamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Manchester United Angel Di Maria kwa kitita cha pauni milioni 44.3.

Raia huyo wa Argentina anaondoka Man United mwaka mmoja baada ya kilabu hiyo kuilipa Real Madrid kitita cha pauni milioni 59.7 ili kumsajili.

Image caption Di Maria

Di Maria mwenye umri wa miaka 27 ametia sahihi mkataba wa miaka minne na mabingwa hao wa Ufaransa baada ya kufanyiwa ukaguzi wa matibabu nchini Qatar siku ya jumanne.''Ninajivunia na ninasubiri kuanza kuvaa jezi za PSG',' alisema Di Maria.