Wilshere kuukosa mwanzo wa msimu

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kiungo wa Klabu ya soka Arsenal,Jack Wilshere

Kiungo wa kimataifa wa Uingereza na Klabu ya soka ya Arsenal, Jack Wilshere atakua nje ya uwanja kwa wiki 6 mpaka 8.

Wilshere amepata ufa katika mfupa wa enka ya mguu wa kulia wakati wa mazoezi siku ya jumamosi .

Kuumia kwa kiungo huyu kutamfanya kuukosa mwanzo wa msimu mpya wa ligi kuu ya England itayoanza jumamosi Agosti 8

Katika msimu uliopita mchezaji huyu alikaa nje ya uwanja kwa miezi mitano akiunguza enka ya mguu wa kushoto.

Tangu ajiunge na Arsenal mwaka 2001 Wilshere amefanyiwa upasuaji mara mbili wa enka kwa miguu yote miwili.