Coutinho anusurika kukaa benchi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Coutinho mwenye kibwenzi akigonga na Luis Suares

Philippe Coutinho alikaribia kutolewa nje kabla ya kushinda asema Rodgers.

Meneja wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers amesema alikaribia kumtoa uwanjani Philippe Coutinho kabla ya kuifunga Stoke. Mbrazili huyo alifunga bao pekee katika mchezo huo baada ya mashambulizi ya mda mrefu kutoka kila upande.

''Unapaswa kumuacha dimbani kwa kadri unavyoweza kwa sababu anastahili'' alisema Rodgers.''Ninafuraha nilimuacha acheze lakini nakiri sikujua nini kingefuata.Ilikua na bahati alipata goli na aliendelea kucheza.''

Timu hizo mbili zilikutana katika mchezo wa mwisho msimu wa 2014-2015 ambapo Stock waliondoka na ushindi mnono wa mabao 6-1.