Chelsea yakata rufaa

Haki miliki ya picha Martin Rickett PA
Image caption Thibaut Courtois

Klabu ya Chelsea inatarajiwa kukata rufaa dhidi ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa mlinda mlango Thibaut Courtois katika mchezo uliopigwa jumamosi dhidi ya Swansea ambao uliisha kwa droo ya magoli mawili katika uwanj wao wa nyumbani Stamford Bridge.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji huyo mwenye umri wa miaka 23 alitolewa nje dakika ya 52 baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji Bafetimbi Gomis wa Swansea ambaye alikua anakwenda kushinda ambapo Swansea walipata penalti kutokana na faulo hiyo.

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alikataa kuongelea uamuzi huo baada ya kipute cha mwisho. Rufaa ya Chelsea itasikilizwa na chama cha soka nchini Uingereza FA siku ya jumanne.

Iwapo rufaa hiyo itakataliwa, Courtois ambaye anatarajiwa kufungiwa mchezo mmoja atakosekana katika safari ya kuwakabili washindi wa pili kwenye msimu uliopita Manchester City jumapili ijayo.

ikumbukwe kwamba,Asmir Begovic aliyesajiliwa kutoka klabu ya Stoke aliichezea Chelsea kwa mara ya kwanza dhidi ya Swansea baada ya kutolewa nje Courtois.