Toure ang'ara katika ushindi wa Man City

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Yaya Toure akiinua mkono kufurahia ushindi

Yaya Toure aliiongoza Man City katika ushindi mnono dhidi ya West Brom ambapo Raheem Sterling aliyesajiliwa majira ya joto kwa dau la pauni milioni 49 akicheza mchezo wake wa kwanza kwa timu yake mpya.

Mkwaju wa Toure uliombabatiza mchezaji mwenzake David Silva ulikwenda pia kwenye miguu ya mlinzi wa West Brom Craig Dawson kabla ya kutinga nyavuni.

City waliendeleza kupanua ushindi wao baada ya Toure kupiga mkwaju mwingine uliokwenda kona ya juu na kuwa goli la pili.Nahodha Vincent Kompany alihitimisha ushindi huo kwa mpira wa kona na kuwa mwanzo mzuri katika dhamira ya kulipata taji la ligi kuu.

West Brom walikua na nafasi chache baada ya mpira wa kona uliopigwa na Chris Brunt kuunganishwa kwa kichwa na James Morrison ambayo ilidakwa vyema na Joe Hart.

City watakua wenyeji wa mabingwa wa amsimu uliopita Chelsea na inawezekana wakamkosa kiungo Yaya Toure aliyetolewa baada ya kupata maumivu ya misuli ya paja.