IAAF kuwachukulia hatua wanariadha 28

Haki miliki ya picha IAAF
Image caption IAAF

Shirikisho la riadha duniani IAAF limesema kuwa linachukua hatua kali dhidi ya wanariadha 28 walioshiriki katika michezo ya dunia ya mwaka 2005 na 2007 baada ya kukagua upya violezo vya mikojo yao na kupata matokeo mabaya.

Shirikisho hilo hatahivyo limesema kuwa halitawataja wanariadha hao kwa sababu za kisheria.

Limesema kuwa ni wachache tu waliosalia katika riadha na kwamba limewasimamisha kutoshiriki katika michezo ya dunia mjini Beijing.

BBC inaelewa kwamba wengi wa wanariadha hao wanatoka Urusi,Belarus,Uturuki na Ukraine.

Ripoti ya wiki iliopita inasema kuwa medali nyingi zilishindwa na wanariadha ambao vipimo vyao vya damu vimekuwa na shauku kubwa.

Shirikisho hilo la riadha lilisema kuwa lilianzisha kukagua tena vipimo vya damu vya wanariadha hao kuanzia mwezi Aprili.