Watuhumiwa mauaji ya mwandishi wakamatwa

Image caption Rasim Aliyev,akipigwa ngumi na polisi

Polisi nchini Azerbaijan imemtia mbaroni mwanamichezo,pamoja na watu wengine watano kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la mauaji ya mwandishi wa habari ambaye alikua akiwakosoa wanamichezo.

Rasim Aliyev aliandika katika mtandao wa kijamii wa facebook kwamba, mwanamichezo Javid Huseynov wa timu ya Gabala anapaswa kufungiwa kushiriki katika michezo baada ya kupeperusha bendera ya Uturuki mbele ya mashabiki wa klabu ya Apollon Limassol wa Ugiriki baada ya mchezo wa ligi kuu ya Europa .

Baada ya kupokea vitisho vya kuuawa,Rasim Aliyev alipigwa na baadae alifariki dunia mwanzoni mwa wiki hii akiwa hospitalini baada ya kupata majeraha makubwa.

Shirika la Usalama na Ushirikiano wa Ulaya (OSCE) limeyalaani mauaji hayo na kutoa wito kwa mamlaka ya kuhakikisha usalama kwa waandishi wa habari na kusema matukio kama hayo yanazorotesha sekta ya habari.