Dzeko ajiunga na kilabu ya Roma

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Dzeko

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Edin Dzeko amejiunga na kilabu ya ligi ya Seria A Roma kwa mkopo.

Kilabu hiyo imetoa kitita cha pauni milioni 2.9, na nyengine pauni 7.9 zikitarajiwa kulipwa iwapo uhamisho huo utabadilika na kuwa wa kudumu.

''Nimekuja hapa kushinda mataji'',alisema Dzeko.

''Ninaweza kuahidi kitu kimoja kwamba nitajitahidi vilivyo katika kilabu hii''.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na kilabu ya Etihad kutoka Wolfsburg mnamo mwaka 2011 kwa pauni milioni 27.

Alikuwa ameweka sahihi ya kandarasi ya miaka minne katika uwanja wa Etihad msimu uliopita.

Hatahivyo,meneja manuel Pelegrini hivi majuzi alikiri kwamba Dzeko alikuwa na uwezo mkubwa kuondoka katika Etihad kufgutia usajili wa RaheemSterling kutoka Liverpool kwa kitita cha pauni milioni 49.