Paulo Wanchope abwaga manyanga

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Eduardo Li rais wa soka Costa Rica

Meneja wa timu ya taifa ya mpira wa miguu wa Costa Rica amebwaga manyanga siku moja baada ya kuhusika na tukio la kupigana wakati wa mchezo huko Panama.Paulo Wanchope mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Costa Rica aliyewahi pia kucheza kwenye ligi kuu nchini Uingereza, alikua akitazama timu yake ya taifa ya vijana walio chini ya miaka (23) wakati vurumai hizo zilipozuka.

Paulo anaonekana katika mkanda wa video akiwa na hasira huku akifungua geti karibu na uwanja ambapo alianza kupambana na bwana mmoja kabla ya wanausalama kuingilia kati.Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa meneja huyo hakua na furaha na muamuzi wa mchezo huo,pamoja na hayo mchezo huo uliisha kwa matokeo ya bila kufungana.