Barcelona yacharazwa 4-0 na Bilbao

Haki miliki ya picha AP
Image caption Barcelona

Kilabu ya Athletico Bilbao iliwawacha mabingwa wa kombe la vilabu bingwa Ulaya mdomo wazi katika awamu ya kwanza ya mechi ya kombe la Super Cup huku Aritz Aduriz akicheka na wavu mara tatu katika mechi isio ya kawaida.

Mikel San Jose alifunga bao la kwanza baada ya dakika 13 na mkwaju uliopigwa kutoka katikati ya uwanja baada ya makosa yaliofanywa na kipa Marc Andre Ter Stegen.

Barcelona ambayo iliwachezesha wachezaji wasio na uzoefu mkubwa baadaye ilifungwa mabao matatu katika kipindi cha mda wa dakika 45 za kipindi cha kwanza,na kuwawacha na jukumu kubwa la kubadilisha mambo katika uwanja wa Nou Camp.

Ni mara ya pili katika mechi mbili ambapo Barcelona wamefungwa mabao manne baada ya ushindi wa 5-4 dhidi ya Sevilla katika kombe la UEFA Super Cup.

Na kushindwa huko kwa Barcelona kunamtia wasiwasi kocha Luis Enrique wakati ambapo timu hiyo inajiandaa kutetea mataji yake matatu iliopata msimu uliopita huku mechi yao ya kwanza katika ligi ikiwa ni ile kati yake na Bilbao katika uwanja wa San Mames.