Djokovic:''Kuna mtu anavuta bangi ''

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Novak Djokovic

Mchezaji nambari moja duniani kwa upande wa Tenisi Novak Djokovic alilalama kwa msimamizi wa mchezo huo kwamba alikuwa akinusa harufu ya bangi katika ukumbi wa mechi ya kombe la Rodgers aliomshinda Jemery Chardy.

Baada ya kushinda seti ya kwanza ,raia huyo wa Serbia alimfuata msimamizi wa mechi hiyo na kusema kuwa, ''Kuna mtu anavuta bangi ,naweza kunusa harufu yake na nasikia kizunguzungu''.

Baadaye Djokovic aliwaambia maripota:''Huwezi kuamini ilivyokuwa ikiniathiri,yeyote ambaye alikuwa akivuta,natumai hatarudi tena kesho,nadhani amejivicha katika mbingu ya saba''.

Djokovic alisema kuwa alinusa harufu hiyo wakati wa mechi yake ya wachezaji wawili kila upande na mwenzake Janko Tipsarevic siku ya ijumaa.

''Jana nilinusa katika mechi ya wachezaji wawili kila upande ,leo tena.Lazima kuna mtu ambaye anajivinjari katika ukumbi huu,alisema.