Mourinho amfanyia masikhara Wenger

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wenger na Mourinho

Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho amemfanyia masikhara mwenzake wa Arsenal Arsene Wenger huku the Blues ikijiandaa kukabiliana na kilabu ya Manchester City siku ya jumapili.

Kocha wa Mancity Manuel Pellegrini alitia mkataba mpya hivi majuzi baada ya kumaliza wa pili katika ligi msimu uliopita.

Na alipoulizwa iwapo alishangazwa na mkataba huo ,Mourinho alisema:kwa nini?Kuna klabu nyengine ambazo wameshindwa kuchukua taji la ligi kuu kwa miaka 15 na meneja hayajabidilishwa.

Arsenal ilishinda kwa mara ya mwisho taji la ligi kuu Uingereza mwaka 2003-2004.

Lakini kocha Arsene Wenger ambaye amekuwa akiisimamia timu hiyo tangu mwaka 1996 ameiongoza miamba hiyo ya London kushinda mataji mawili ya kombe la FA mfululizo.

Wenger vilevile alifanikiwa kuishinda Chelsea kwa mara ya kwanza katika mechi 14 chini ya Mourinho katika Kombe la Charity Shield.