Liverpool waichapa Bournemouth EPL

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mshambuliaji wa Liverpool, Christian Benteke

Liverpool imepata ushindi wa pili katika michuano ya ligi ya England dhidi ya timu ya Bournemouth,Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani Anfield

Bao pekee la ushindi la majogoo wa Anfield liliwekwa kimiani na mshambuliaji mpya wa timu hiyo Mbelgiji Christian Benteke katika dakika ya 26 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na kiungo Jordan Henderson.

Kwa ushindi huu timu hiyo inasogea mpaka nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 6 na mabao mawili.

Huku Bournemouth wakisalia nafasi ya 19 wakiwa hawana alama hata moja baada ya kucheza michezo miwili ya ligi.