Ramos asaini mkataba mpya

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Beki wa Real Madrid Sergio Ramos

Beki wa klabu ya soka ya Real Madrid Sergio Ramos, amesaini mkataba mpya na timu yake.

Ramos mwenye umri wa miaka 29, amesaini mkataba wa miaka mitano utakaomuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2020.

Mlinzi huyu alikua anahusishwa kujiunga na miamba wa soka wa England klabu ya Manchester United kama sehemu ya mabadilishano na kipa anayewindwa na Real David De Gea.

Baada ya kusaini mkataba huo Ramos amesema “ Mawazo yangu ni kuwa hapa na kustaafu soka nikiwa hapa kama raisi wa timu ataruhusu,nashukuru nina changamoto mpya nikiwa nahodha wa timu” .